The Missionary Society of St. Francis De Sales

The Missionary Society of St. Francis de Sales (Fransalians), is an international missionary organisation, founded in the year 1838 in Annecy, in France by a Catholic Priest, Fr. Peter Mermeir. The society aims to live and proclaim a way of life following Jesus Christ, helping the poor, and to educate and form the young generation for a better tomorrow. There are over 100 schools and colleges run by the MSFS in different parts of the world. The society is present in Europe, America, South America, Australia and Africa. In Africa we work in Tanzania, Kenya, Uganda, Namibia, South Africa, Mozambique, Chad, Zambia, Malawi, and Cameroon.

The Missionary Society of St. Francis de Sales came to Tanzania in 1988 and started their work in the Tabora Region. From the first mission in Tabora, the congregation grew to become the Province of East Africa that engages in evangelisation, education and social work in Tanzania, Kenya and Uganda.

The educational establishments of the society in Tanzania include; De Sales primary school Isaka, St. Francis De Sales primary school in Kagongwa, SFS vocational training Institute (Shinyanga Region), Fransalian mission School, Ipuli, St. Francis De sales, secondary school, Ipuli, St. Francis De Sales Primary school, Bukene (Tabora Region), St. Francis De Sales Primary school, Kingurunyembe, St. Francis De Sales Primary School, Dumila, St. Francis De Sales Seminary (Morogoro Region), Fransalian Hekima Secondary School, Maji ya Chai (Arusha Region),  the Fransalian Mission School, Mkuza (Pwani Region), and the Fransalian Mission school, Bombambili (Dar es Salaam Region).

Shirika la Wamisionari wa Mtakatifu Fransisko wa Sales         

Shirika la Wamisionari wa Mtakatifu Fransisko wa Sale (Wafransaliani) ni shirika la kimataifa la misionari lililoanzishwa mwaka 1838 huko mji wa Annecy nchini Ufaransa na Padre Mwenyeheri  Peter Mary Mermeir.  Malengo ya shirika la Mt. Fransisko wa Sales (MSFS) ni kuishi na kutangaza njia ya maisha katika ubinafsi wa Yesu Kristu, kuwasidia maskini, na kuwaelimisha na kuunda kizazi kipya kwa ajili ya maisha bora ya kesho. 

Wamisionari wa Mt. Fransisko wa Sales wanaendesha shule na vyuo Zaidi ya 100 (mia moja) sehemu mbalimbali duniani. Shirika lipo Ulaya, Marekeni, Amerika ya kusini, Australia na Afrika. Barani Afrika Shirika lipo katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Namibia, Afrika ya kusini, Msumbiji, Chadi, Zambia, Malawi, na Kameruni.

Shirika la Wamisionari wa Mt. Fransis De Sales lilikuja Tanzania 1986 na kuanza kazi katika Jimbo Kuu la Tabora. Tangu mwanzo shirika kujihusisha na shughuli za kuwaimarisha watu kiroho, kuelimisha na kufanya shughuli za kijamii.  Uboreshaji wa elimu katika jamii ya Tanzania ulihusisha kuanzishwa kwa shule zifuatazo:

  • Shule ya msingi ya De Sales, Isaka (Mkoa wa Shinyanga)
  • Shule ya msingi ya Mt. Fransisko wa Sales, Kagongwa (Mkoa wa Shinyanga) 
  • Chuo cha ufundi stadi SFS (Mkoa wa Shinyanga)
  • Shule ya msingi ya Fransaliani, Ipuli, (Mkoa wa Tabora)
  • Shule ya sekondari ya Mt. Fransisko wa Sales, Ipuli (Mkoa wa Tabora)
  • Shule ya msingi ya Mt. Fransisko wa Sales, Bukene (Mkoa wa Tabora)
  • Shule ya msingi ya Mt. Fransisko wa Sales, Kigurunyembe, (Mkoa wa Morogoro)
  • Shule ya msingi ya Mt. Fransisko wa Sales, Dumila (Mkoa wa Morogoro) 
  • Seminari ya Mt. Fransisko wa Sales (Mkoa wa Morogoro)
  • Shule ya Sekondari Fransaliani Hekima Maji ya Chai (Mkoa wa Arusha )
  • Shule ya  Fransaliani Mkuza (Mkoa wa Pwani)
  • Shule ya Fransaliani Bombambili (Mkoa wa Dar es Salaam)